Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha

( AUWSA )

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 13.5 KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SAFI SINYA - NAMANGA

Imewekwa: 16 April, 2025
RAIS SAMIA ATOA BILIONI 13.5 KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SAFI SINYA - NAMANGA

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 13.5 KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SAFI SINYA - NAMANGA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo tarehe 14 April, 2015 ameshuhudia utiaji saini wa mradi mkubwa wa maji safi wa Sinya - Namanga wenye thamani ya shilingi bilioni 13.5katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Ildonyo, kata ya Sinya Wilaya ya Longido

Mhe. Makonda amesema kuwa hatua hiyo inaenda kufingua ukurasa mpya kwa wananchi wa maeneo hayo kwa kwani sasa watakuwa na matumaini ya kupata huduma ya maji kwa karibu.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. samia Suluhu Hassan kuwa kinara wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji kwa kuwa yeye ni mama na anatambua changamoto wanazopitia akina mama ikiwemo kutembea umbali mrefu kufuata maji.

Hata hivyo amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutekeleza majukumu yake kwa wakati ili wananchi kupata huduma hiyo muhimu ndani ya muda walioahidiwa na viongozi wao sambamba na Wananchi kutokuwa kikwazo kwa mradi kutokukamilika kwa wakati kwa kutoa ushirikiano na kuwa waaminifu hasa kwa vijana watakaopata fursa ya ajira katika mradi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira AUWSA Jiji la Arusha, Mhandisi Justine Rujomba, amesema kuwa Kwasasa Maji yanayozalishwa kutoka chanzo cha Mto simba kilichopo Wilaya ya Siha mkoani kilimanjaro ni lita milioni milion 1.7 ambapo mahitaji ni lita milioni 3.8 na Kisima ambacho kimechimbwa kwenye eneo hilo kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.4 kwa siku na kufanya uzalishaji wa maji katika maeneo hayo kufikia wastani wa lita milioni 4.1 kwa siku.

Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Zongii construction limited na unatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya elfu 37 huku mradi ukitarajiwa kukamilika mwezi juni 2027 na Wananchi wa eneo hilo watapewa kipaumbele cha kupata maji ndipo yasambazwe kwenye maeneo mengine.